RONALDO APIGA HAT-TRICK YA 39 REAL MADRID IKIICHINJA ATLETICO MARDID 3-0 NYUMBANI KWAO


ATLETICO MADRID imenyamazishwa nyumbani na Real Madrid katika mchezo wa La Liga ulioshuhudia Cristiano Ronaldo akifunga mabao matatu katika ushindi wa 3-0 ndani ya dimba laVicente Calderon.

Hii inakuwa ni mara ya 39 kwa Ronaldo kufunga mabao matatu katika mechi moja (hat-trick) huku pia akitimiza mabao 18 dhidi ya Atletico na kuvunja rekodi ya mwaka 1960 iliyowekwa na gwiji  Alfredo Di Stefano aliyefunga mara 17 dhidi ya watani wao hao wa jiji la Madrid.

Ronaldo alifunga bao la kwanza kwa free kick kunako dakika ya 23 kabla hajafungwa kwa penalti dakika ya 71 na dakika sita baadae akatupia bao la tatu kufuatia krosi tamu ya Gareth Bale.

Kwa ushindi huo, Real Madrid sasa inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi nne.

Atletico Madrid: Oblak 7, Juanfran 5.5, Savic 4, Godin 5, Filipe Luis 6, Gabi 6.5 (Correa 62, 5.5), Koke 5, Saul 5, Carrasco 5.5, Torres 4 (Gameiro 62, 5), Griezmann 5.5

Real Madrid: Navas 6, Carvajal 6.5, Nacho 6, Varane 6.5, Marcelo 7.5, Vazquez 7 (Asensio 86), Kovacic 7, Modric 7, Bale 7, Isco 8 (Benzema 79), Ronaldo 9.5 (James 82)
Cristiano Ronaldo celebrates after completing his hat-trick in Real Madrid's emphatic derby win against their bitter rivalsCristiano Ronaldo akionyesha mbwembwe zake baada ya kufunga bao la tatu
Ronaldo poses in front of the cameras after dispatching his penalty beyond Jan Oblak and into the back of the netRonaldo baada ya kufunga bao la pili kwa penalti
The Portuguese star celebrated his opening strike in typically flamboyant style in front of the opposition supportersRonaldo akishangilia bao la kwanza

No comments