ROSE NDAUKA: WASANII ANDAENI KAZI BORA KWA WINGI HATA KAMA HAZILIPI

KIMWANA wa Bongomuvi, Rose Ndauka amesema kuwa kukata tamaa katika maisha ni adui wa mafanikio na kuwataka wasanii wenzake kukaza buti kwa kuandaa kazi bora zaidi hata kama filamu hazilipi.

“Binafsi siamini kwamba Bongomuvi imekufa ila upepo mchafu umepitia soko la filamu nchini. Wasanii wanapaswa kukaza buti kwani kukata tamaa katika maisha ni adui mkubwa wa mafanikio,” alisema Ndauka.

Alisema, kinachotakiwa ni wasanii kutambua changamoto katika maisha ni za kawaida na wanatakiwa kutafuta njia za kukabiliana nazo na sio kukata tamaa.


Mwigizaji huyo alisema ni vyema kutafakari ni wapi wamekosea na kufanya marekebisho na kuirudisha Bongomuvi kwenye chati kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

No comments