RUBY ASHANGAA KUPAKAZIWA KUJIPENDEKEZA “WCB”

STAA wa muziki wa Kizazi Kipya Hellen George “Ruby” anaamini kwamba akiwa karibu na Diamond Platnumz anaweza kujifunza vitu vingi vinavyoweza kumsaidia katika muziki wake.

Kutokana na hilo, alisema kuwa amekuwa akimfuata kila mara lakini sasa anashangaa kusikia baadhi ya watu walkidai kwamba anataka kujiunga na lebo ya Wasafi Classic Baby “WCB”.

“Nikiwa na Diamond ninajifunza vitu vingi, hiyo haina maana kwamba nikiwa nae nimejiunga WCB… pale kuna Studio na kuna mtayarishaji wa muziki, Lizer, watu tunataka kufanya nae kazi,” alisema Ruby.


Msanii huyo anayeendelea kutamba na wimbo wake wa “Walewale” ambao umezua minong’ono kwamba ameutunga kuushambulia uongozi wake wa zamani, jambo ambalo amekuwa akilikanusha.

No comments