Habari

RYAN GIGGS ASEMA JUAN MATA NI KIFAA MUHIMU MANCHESTER UNITED

on

RYAN GIGGS amesema Juan Mata ni mchezaji muhimu kwa Manchester United na kumwelezea kama mtu mwenye uwezo wa kufunga na kutengeneza magoli.
Giggs alifanya kazi na nyota huyo wa Hipsania wakati alipokuwa kwenye benchi la ufundi chini David Moyes na Louis van Gaal.
Manchester United ilimnunua Mata kwa pauni milioni 37 kutoka Chelsea katika usajili wa dirisha dogo la Januari 2014.
Hatma ya Mata ilikuwa mashakani baada ya Jose Mourinho kupewa kibarua cha kuinoa klabu hiyo msimu huu, lakini mambo yakawa kinyume chake ambapo sasa kiungo anafurahia maisha Old Trafford chini ya kocha huyo Mreno. Mourinho ndiye aliyemuuza Mata kwa United wakati alipokuwa akiikochi Chelsea.
“Ni mchezaji mzuri. Anatengeneza magoli, anafunga magoli”
Akiongea na ITV, Giggs alisema: “Ni mchezaji mzuri. Anatengeneza magoli, anafunga magoli, ni mtu anayeheshimu majukumu yake”.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *