SAFINA WA MIZENGWE AWATAKA WASANII WAISAIDIE SERIKALI KUPAMBANA NA WIZI WA KAZI ZAO

MCHEKESHAJI wa kundi la Mizengwe Jesca Kindole  “Safina” amewataka wasanii kuunga mkono juhudi za serikali za kudhibiti vitendo vya wizi wa kazi zao ili hatimae waweze kufaidi jasho lao.

Safina alisema kuwa sanaa ni ajira kwa baadhi ya watu, hivyo yangetengenezwa mazingira mazuri ili wasanii wanufaike na pia serikali iweze kupata kodi kuliko ilivyo sasa ambapo faida inaishia mikononi mwa wachache.

Msanii huyo alisema kuwa asanii wengi wa Tanzania wanaishi kimasikini kutokana na kudhulumiwa jasho lao, hivyo umefika wakati wa kuunga mkono juhudi za serikali ili kukomesha mchezo huo.


“Juhudi ziongezwe zaidi kwani sanaa inalipa ila wizi na unyonyaji uliopo unatufanya wasanii wengi tuishi kimasikini tofauti na jasho tunalolitoa,” alisema Safina.

No comments