SHAMSA FORD ASEMA HAWEZI KUFICHA NAMNA ANAVYOMPENDA MUME WAKE

SHAMSA Ford amesema kuwa ni bora aonekane mshamba mbele ya jamii lakini hataweza kuficha hiasia zake za mapenzi kwa mumewe kwa vile ndiyo alivyoumbwa.

 “Kuna muda huwa natamani dunia nzima ijue ni jinsi gani nakupenda na kukuthamini kwa sababu mimi ni mwanamke nisiyeweza ficha hisia zangu hata mkiniona mshamba,” aliandika Shamsa kupitia Instagram na kuendelea.

“Ulikutana na wasichana wengi katika maisha yako lakini ni mimi pekee ndiye niliyepata bahati ya kuwa mke wako." 

"Naomba niseme naheshimu siku uliyonitolea barua naheshimu siku uliyonitolea mahari, lakini kubwa kuliko vyote naheshimu siku uliyoapa ndani ya nyumba ya Mungu kuwa mimi ndiyo mke wako.”

Alisema kwa hakika Mungu ndiye aliyewaunganisha na kwa kudra zake watazikana.

No comments