SHOLO MWAMBA: KWANZA MUZIKI, MAPENZI NA NDOA BAADAE

MKALI wa muziki wa Singeli, Seif Mwinyijuma “Sholo Mwamba” amesema kuwa hawezi kuoa kwa sasa na badala yake ameelekeza nguvu kwenye muziki hadi hapo baadae.

Sholo Mwamba alisema kuwa mipango ya kuoa ipo na haitafutika hata kidogo, lakini kwa sasa ameamua kukuza muziki wake kwanza ili aendelee kufanya vizuri zaidi.

“Nina mchumba lakini siwezi kuoa kwa sasa kwani anaishi kwao na mimi niko peke yangu, lakini sababu kubwa ya kutooa mapema ni kutaka kuelekeza nguvu katika muziki wangu kwanza,” alisema Sholo aliyeshirikishwa na Profesa Jay katika wimbo wa “Kazi Kazi.”


Alisema kuwa muziki wa Singeli unatakiwa kuenea nchi nzima, kwa maana hiyo ni lazima ajipe muda wa kutosha wa kujiimarisha katika muziki huo ndipo mambo mengine yafuate.

No comments