SHUJAA OLIVIER GIROUD ALA “BATA” NA DAVID BECKHAM

BAADA ya kukiokoa kikosi cha Arsenal katika mchezo wa majuzi dhidi ya Manchester United straika Olivier Giroud ameonekana akiponda raha na bishoo David Beckham.

Giroud alifunga bao pekee la Arsenal lililoipa timu hiyo sare ya bao 1-1 katika mtanange huo dhidi ya Mancherter United uliochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford.

Baada ya matokeo hayo mchezaji wa zamani wa Arsenal Robert Pires alitupia picha kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii akiwa na mastaa Giroud Santi Cazorla na Beckham.


Wachezaji hao wanne walikuwa katika hafla iliyoandaliwa na mfuko wa Giroud ambao una lengo la kuwasaidia akina mama na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

No comments