“SINA MPANGO WA KUANIKA MALI ZANGU KWENYE MITANDAO YA KIJAMII” AFUNGUKA ALI KIBA

NYOTA wa muziki wa Kizazi Kipya, Ali Kiba amesema kuwa hafikirii na hana mpango wa kuonyesha mali zake kwenye mitandao ya kijamii kwa madai kwamba haoni umuhimu wa kufanya hivyo.

Kib alisema kuwa wanaomsema kuwa hana kitu waendelee kufanya hivyo lakini kamwe hawezi kuishi kama watakavyo bali anaishi anavyotaka yeye mwenyewe.

“Kama nina mali ni zangu mwenyewe na kama sina kitu pia hayo ni maisha yangu mwenyewe, kwanini nikatangaze kwenye mitandao ya kijamii? Ninaishi nitakavyo sio watakavyo hao wanaonisema,” alisema.


Kiba wiki iliyopita alipewa tuzo yake ya MTV EMA ya Best International Act aliyoshinda baada ya awali kukabidhiwa kimakosa kwa Wiz Kid wa Nigeria.

No comments