SNURA WA MAJANGA AMMWAGIA SIFA "CHURA" MPYA

SNURA Mushi amesema kuwa wimbo wake wa "Chura" alioufanyia mabadiliko una mashabiki wengi kuliko ule wa kwanza na hivyo ana uhakika ataendelea kuvuna pesa kupitia wimbo huo.

Alisema alipoutoa kwa mara ya kwanza kabla kuzuiwa na serikali ulitazamwa mara 53,174 kwa kipindi kifupi lakini huu wa sasa umetazamwa zaidi ya mara 90,000 ndani ya kipindi kifupi.

“Hii inaonyesha kuwa Chura mpya ni zaidi wa yule wa kwanza hivyo nina uhakika nitaendelea kubamba mashabiki na sababu kubwa ni kwamba wimbo huo ulitokea kupendwa tangu mwanzo,” alisema Snura.


Alisema kuwa anaishukuru serikali kwa jinsi ilivyomrekebisha na sasa ana uhakika wa kufanya kazi zake kwa umakini na kuwasaidia wasanii wenzake kuandaa nyimbo kwa kuzingatia maadili.

No comments