SUSO ASEMA AMEDHIHIRISHA THAMANI YAKE BAADA YA KUFUNGA MABAO MAWILI KATIKA “DERBY” YA ITALIA


BAADA ya kufunga mabao mawili katika derby ya Italia straika wa AC Milan Suso amesema kuwa sasa amedhihiriasha thamani yake kwa vinara hao wa Ligi ya serie A.

Katika mchezo huo majuzi Suso aliifungia AC Milan mabao mawili yaliyoyafanya watoke sare ya mabao 2-2 dhidi ya mahasimu wao, Inter Milan ambao walisawazisha bao lao dakika ya 92.

Msimu uliopita nyota huyo raia wa Hispania alicheza mechi moja kabla ya kupelekwa kukipiga kwa mkopo katika timu ya Genoa lakini kwa sasa anaonekana kutakata chini ya kocha Vincenzo Montella anayekinoa kikosi hicho cha viunga vya San Siro baada ya kufunga mabao manne katika mechi 13 na kuifanya AC Milan kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi ikifuatana na pointi na AS Roma inayoshika nafasi ya pili.

“Nilitaka nipate nafasi nikiwa chini ya Mihajilivci lakini mambo yakaenda vibaya,” Suso aliuambia mtandao wa Mediaset Premium.


“Nikaenda Genoa ili kumdhihirishia kila mmoja kuwa nina thamani AC Milan na sasa tupo katika msitari mzuri lakini bado kuna safari ndefu,” aliongeza nyota huyo.

No comments