THEA ASEMA BONGOMUVI INAHARIBIWA NA WASANII WAUZA SURA, WATAFUTA KIKI

MKONGWE wa filamu Ndumbagwe Misayo “Thea” ameibuka na kusema kuwa Bongomuvi inaharibiwa na baadhi ya wasanii ambao kazi yao ni kuuza sura tu na kutafuta kiki bila kuwa na uzoefu wa kuigiza.

Alisema kuwa hao ndio wamekuwa wakisababisha Bongomuvi idharauliwe na pia ionekane imekufa, ilihali wapo wasanii wenye uwezo mkubwa ambao wanafanya kazi vizuri.

“Sitaki kuwataja kwa majina lakini kwa wanaofuatilia filamu za Kitanzania watakuwa wanawajua wasanii ambao kazi yao ni kuuza sura tu na kutengeneza kiki ili wapate umaarufu,” alisema Thea.


Alisema kuwa bahati nzuri wengi wanaofanya kazi zao vizuri wameshawashitukia na sasa huwa hawawashirikishi katika filamu na hivyo kuwafanya wajiondoe wenyewe mmoja baada ya mwingine.

No comments