Habari

THIBAUT COURTOIS AZITOLEA NJE ATLETICO, REAL MADRID… asema anajisikia furaha kubwa kuwepo Chelsea

on

MLINDA mlango Thibaut Courtois
amezitolea nje timu mbili za La Liga ambazo zilikuwa katika orodha ya
kumwania katika usajili wa dirisha la Januari mwakani.
Akikanusha mlinda mlango huyo
alisema pamoja na kuakiwa na timu za Atletico na Real Madrid msimamo wake ni
kutotaka kurejea kukipiga katika Ligi hiyo ya Hispania.
Kutokana na hilo Thibaut
amesisitiza dhamira yake ya kutaka kubakia ndani ya kikosi cha matajiri wa
Darajani Chelsea.
Courtois mwenye umri wa miaka
24 aliitumikia kwa mkopo Atltico Madrid na kuisaidia kushinda mataji ya Winning
La Liga ikiwemo ubingwa wa Copa del Rey na ubingwa wa Ligi ya Ulaya.
Pia aliisaidia Atletico kufikia
fainali ya Ligi ya Mabingwa ya Ulaya mnamo mwaka 2014.
Akinukuliwa mlinda mlango huyo
amesema kwa sasa anajivunia hatua ya kuaminika kama nambari moja ndani ya Chelsea hatua inayompa faraja kubwa.
“Ninachoweza kusema ni kwamba
sijazungumza na timu yoyote kati ya Atletico ama Real Madrid hivyo taarifa zote
za uvumi ni uzushi mkubwa.”

“Nina jisikia furaha kuwepo
hapa Chelsea nina heshima kubwa hapa hivyo sitarajii kuondoka kwa sasa.”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *