TID ASEMA HANA MPANGO QWA KUIGA MUZIKI WA NJE

MKONGWE wa muziki wa Bongofleva Khaleed Mohammed a.k.a "TID" ambaye sasa anatamba na kibao chake cha “Confifdence” amesema hana mpango wa kuiga muziki wa nje kwa madai kwamba kufanya hivyo kunapoteza uhalisia wa muziki huo.

Alisema kuwa baadhi ya wasanii wakiwamo wanaochipukia wamekuwa wakiiga muziki wa nje na kusababisha Bongefleva kupoteza mizizi ya muziki huo.


“Muziki wa bongofleva umetokana na mchanganyiko wa muziki wa HipHop na R&B lakini ajabu ni kwamba baadhi ya wasanii sasa wanataka kuimba kama Wanaigeria na kusahau kuwa Bongofleva ni mchanganyiko wa muziki wa HipHop na R&B,” alisema TID.

No comments