TIMBULO ASEMA KWAKE YEYE BADO SANA KUHANGAIKIA SOKO LA NJE

MSANII wa Kizazi Kipya Timbulo amesema kuwa hawezi kupoteza muda kuhangaika soka la nje wakati bado kuna mashabiki hapa nchini mwanaohitaji muziki wake.

“Wakati wasanii wengine wakiangaika kutafuta soko la nje mimi nitaendelea kuwa wa hapahapa kwani huo ndio utofauti wangu na wasanii wenzangu wa muziki huu wa Kizazi Kipya,” alisema Timbulo.


Alisema kuwa hawezi kufanya muziki kwa kufuata mkumbo tu bali anaangalia ni wapi soko lilipo ndiko anakoelekeza nguvu zake na ana uhakika na kile anachokifanya.

No comments