WALINZI WA FEYENOORD KUWEKA “DORIA” OLD TRAFFORD

TIMU ya Manchester United inatarajia kuwapokea walinzi wa timu ya Feyenoord ili kuimarisha hali ya usalama wakati timu hizo zitakapokutana kwenye uwanja wa Old Trafford.

Man United watakuwa nyumbani kuccheza na Feyenoord katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Europa utakaochezwa kesho.

Mashabiki wapatao 7,000 wa klabu hiyo ya Uholanzi wanatarajia kwenda nchini England kuangalia mechi hiyo.

Hatua hiyo ya kuimarisha ulinzi imefanikiwa na viongizi wa timu zote mbili baada ya picha za mashabiki wa Feyenoord kuonekana wakishambuliana na mashabiki wa timu ya Nancy ya Ufaransa wiki iliyopita.


Kwa mujibu wa Daily Mail walinzi 25 watasajiliwa toka Uholanzi ili kujichanganya na mashabiki kuhakikisha hakuna fujo zitakazotokea wakati wa mchezo huo.

No comments