WANAOMSIMANGA WEMA SEPETU KUHUSU KUKOSA MTOTO WAMBOA FAIZA ALLY

MWIGIZAJI filamu Faiza Ally amesema anakerwa na tabia ya baadhi ya watu ambao hupenda kuwasema vibaya wenzao na kuwataka wajifunze kumwogopa Mungu.

“Hakuna kitu ambacho huwa kinanikera kama watu wanaomtukana Wema kuhusu mtoto… ninachukia na sipendi. Hivi ninyi mliozaa mnajua mmezaa kina nani?” alihoji Faiza.

Alisema ni bora kutokuza kuliko asiyejua amezaa mtu wa aina gani kwani inawezekana akawa amezaa jambazi, shoga ama mtu yeyote asiye na faida katika jamii na kwamba ni bora wakakaa wakawaombea watoto wao mema badala ya kumkashifu mtu ambaye hajazaa.


Faiza amewataka wale wanaomsema vibaya Wema kwa kutopata mtoto wakae na waombee vizazoi vyao kwani hawajui walivyozaa vitakuwa kina nani na huenda bora Wema ambaye hajazaa.

No comments