"WASANII WA BONGOFLEVA WAMESHINDWA KUTUMIA VIONJO VYAO WENYEWE" JAY MOE

MUZIKI wa Kizazi Kipya umeelekea kupoteza asili yake kwa sababu wasanii wengi wa Bongofleva wameshindwa kutumia vionjo vyao wenyewe na kuanza kuimba kama wenzao wa nje, kwa mujibu wa Jay Moe.

Rapa huyo amesema wasanii kwenda kurekodi nje ya nchi ni jambo jema kwavile hatua hiyo inasaidia kuongeza soko la muziki wao, lakini tatizo linakuwa kwenye kuiga vionjo.

Msanii huyo ambaye amerudi kwenye gemu akiwa na wimbo “Pesa Madafu” alisema wasanii waendelee kwenda Nigeria na Afrika Kusini lakini wakizingatia kutumia vionjo vyao ambavyo vinasaidia kuitangaza Tanzania.


“Kwa sasa ninajipanga kuibua vipaji vya kina Nikki Mbishi Climax kwa kushirikiana na P-Funk kwa kutoa albamu ambayo itasambazwa mikoa mbalimbali hapa nchini,” alisema Jaymoe.

No comments