WEMA SEPETU ADAI MASHABIKI NAO HUCHANGIA KUGOMBANISHA WASANII

WEMA Sepetu amewataka mashabiki wa filamu kuepuka mtindo wa kutoa taarifa ambazo zinaweza kugombanisha wasanii na badala yake wawe mstari wa mbele kuwaunganisha.

Alisema wapo baadhi ya mashabiki ambao wamekuwa wakifurahia kuona wasanii wakitengana na kununiana, jambo ambalo anaona halifai kupewa nafasi.

“Ninasema hivyo kwasababu kuna watu walikuwa wakizusha maneno kwenye mitandao ya kijamii kwamba mimi na Aunt Ezekiel hatuelewani wakati hakuna ukweli wowote katika hilo,” alisema Wema.


Alisema kuwa suala la watu kutofuatana kimawazo na kimtazamo ni la kawaida na wala haliwezi kuchukuliwa kama hawaelewani na kwamba wanaoeneza uzushi huo wana lengo lao binfisi.

No comments