YEAH TMK MODERN TAARAB KUFICHULIWA RASMI DISEMBA 17 DAR LIVE


HATIMAYE ile kiu ya kuliona kundi jipya la miondoko ya taarab – Yeah TMK Modern Taarab, itakatwa rasmi Disemba 17.

Boss wa kundi hilo, Said Fela ameiambia Saluti5 kuwa Yeah TMK Modern Taarab itazinduliwa Jumamosi ya Disemba 17 ndani ya Ukumbi wa Dar Live jijini Dar es Salaam.

Ujio wa bendi hiyo unafuatia kambi ya nguvu ya takriban mwezi mmoja na nusu, hatua iliyozalisha nyimbo mbili kali “Sina Pupa” wa Bi Mwanahawa Ali na “Kibaya Kina Mwenyewe” wa Aisha Vuvuzela.

Yeah TMK inaundwa na wasanii wengi waliojiengua kutoka Jahazi kama vile Mohamed Mauji, Chidy Boy, Babu Ali, Fatma Mcharuko na Vuvuzela.

Wakali wengine wanaounda kundi hilo ni mtu na dada yake – Omar Teggo na Mauwa Teggo.

No comments