ZLATAN IBRAHIMOVIC ATAMBA KUENDELEA KUNG'ARA OLD TRAFFORD

STRAIKA Zlatan Ibrahimovic amesema kuwa anavyoamini ataendelea kung’ara akiwa na klabu yake ya Manchester United baada ya kuthibitisha nia yake ya kuendelea kukipiga Old Trafford kwa msimu wa pili.

Wakizungumza mauzi wakati wa kijiandaa na mechi ya Man United katika michuano ya Ligi ya Europa dhidi ya Feyenoord iliyopigwa usiku wa kuamkia jana, Jose Mourinho na Ibrahimovic walisema kuwa kuna mpango wa kumpa staa huyo nyongeza ya mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa.

Tangu ajiunge na mashetani hao wekundu akiwa mchezaji huru akitokea katika timu ya PSG mwishoni mwa msimu uliopita, tayari Ibrahimovic ameshafunga mabao manane katika mechi 17 alizokwishawachezea vinara hao.

Hata hivyo mabao mawili aliyoyafunga katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Swansea City kabla ya mapumziko ya kupisha mechi za timu za taifa yalikuwa ni ya kwanza katika michuano ya Ligi Kuu England katika kipindi cha miezi miwili.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari nchini Uholanzi ni kwanini kwa sasa hatakati akiwa na Man United, staa huyo wa zamani wa timu ya Ajax, Barcelona na AC Milan kama kawaida yake alijibu kwa mzaha akisema.

“Huwa nang’aa kwa saa 24, hivyo inategemea ni wakati gani unataka nifanye hivyo.”

“Nimekuwa ndani ya soka kwa muda wa miaka 20 na ndio nimezeeka lakini kwa uzee wangu nimekuwa Napata kitu bora kama ninavyojisikia,” aliongeza nyota huyo matata.

No comments