ALLY CHOCKY ‘AIZIKA’ EXTRA BONGO …asema hana mpango wa kuondoka Twanga Pepeta hata mkataba wake ukiisha


MWIMBAJI mahiri wa African Stars Band “Twanga Pepeta”, Ally Chocky amesema hana mpango wa kuihama bendi hiyo ambayo ana mkataba wa kuitumikia hadi mwaka 2018.

Akiongea na Saluti5, Chocky alisema hata mkataba huo ukiisha bado ataendelea kuitumikia Twanga Pepeta.

Mwimbaji huyo amekuwa akihusishwa kwa nguvu na tetesi za yeye kuifufua bendi yake ya zamani - Extra Bongo.

Akizungumzia suala la Extra Bongo, Chocky alisema hana mpango wa kuifufua bendi yake hiyo ya zamani na badala yake Extra Bongo itabakia kama kampuni ya kuandaa matukio ya burudani na si zaidi ya hapo.

“Sina mpango wa kufufua  Extra Bongo, sifikirii kabisa kumiliki bendi kwa sasa hivi. Nitabakia Twanga Pepeta hata pale mkataba wangu utakapomalizika,” alisema Chocky.

No comments