ANTONIO CONTE AMTAKA MLINZI WA AC MILAN KUIMARISHA KIKOSI CHAKE

KLABU ya Chelsea imeongeza jina la mlinzi kisiki wa klabu ya soka nchini Italia, AC Milan, Gabriel Paletta katika orodha ya wachezaji inaowahitaji kuimarisha kikosi.

Chelsea ambayo inafundishwa na Antonio Conte inataka kuimarisha safu yake ya ulinzi katika harakati zake za kutaka kutwaa ubingwa wa msimu huu.

Akinukuliwa, Conte alisema azma yake ni kufanya usajili wa nguvu kwa ajili ya kuhimili mikiki ya Ligi ya Premier ambayo imejaa ushindani mkubwa.


“Ninahitaji kuwa na kikosi bora na imara. Palatta ni miongoni mwa wanandinga ninaodhani wanakuja kuongeza uimara wa kikosi.”

No comments