ARENE WENGER AKANA KUMBEBA OZIL KWA KUMPA KAZI "ROJOROJO" DIMBANI

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amepinga madai kuwa amekuwa akimpa majukumu mepesi nyota wa timu hiyo Mesut Ozil.

Ozil amekuwa akilaumiwa kwa kutojituma wakati Arsenal inapokuwa na wakati mgumu kwenye mechi mbalimbali.

Kuna picha za Televisheni zilisambaa zikimwonyesha akitembea wakati Arsenal ikishambuliwa na Manchester City kwenye mechi za Ligi Kuu England hivi karibuni.

Arsenal ilifungwa mabao 2-1 kwenye mechi hiyo.

“Nafahamu kuwa Ozil ni hatari zaidi anapokuwa na mpira ila haina maana kuwa hatakiwi kukaba pale tunapopoteza mpira, ana jukumu hilo sawa na wengine,” alisema Wenger.


Wenger alisema kuwa amesikia taarifa hizo za kumponda Ozil lakini anaamini kuwa suala la kusaka mpira ni la wachezaji wote.

No comments