Habari

ARJEN ROBBEN ASEMA HAKUNA NAMNA MEMPHIS DEPAY NI LAZIMA AONDOKE MANCHESTER UNITED

on

WINGA wa Bayern Munich Arjen Robben amesema Memphis Depay anapaswa kuondooka Manchester United na kwenda klabu itakayompa nafasi ya kucheza ili kufufua kipaji chake.
Depay aliwasili Old Trafford kiangazi cha mwaka 2015 chini ya kocha  Louis van Gaal kwa ada ya pauni milioni 25 akitokea  PSV Eindhoven.
Kinyume na matarajio ya wengi kuwa Depay angekuwa tegemeo Manchester United, winga huyo wa Uholanzi ameshindwa kabisa kung’ara Old Trafford ambapo msimu huu chini ya Jose Mourinho amecheza mechi nne tu za Premier League tena akitokea benchi.
Robben ambaye amecheza na Depay kwenye kikosi cha Holland anaamini nyota huyo wa miaka 22 bado ana nafasi ya kuchanua iwapo tu ataondoka Manchester United.
“Ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu,” Robben aliuambia mtandao wa Goal.
“Matunda yake bado hayajaonekana Manchester United hadi hivi sasa. Anacheza mechi chache sana. Nategemea jambo fulani litatokea hapo baadae, pengine ataondoka usajili wa dirisha dogo”.
Arjen Robben still believes Depay can reach his huge potential if he leaves Manchester United

Arjen Robben (kulia) bado anaamini Depay (kushoto) ana nafasi ya kufufua kipaji chake iwapo ataondoka Manchester United

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *