ARSENAL YAANGUSHA KARAMU YA 5-1 KWA WEST HAM … Sanchez apiga hat-trickARSENAL imetoa onyo kali kwenye Ligi Kuu ya England baada ya kuitungua West Ham 5-1.

Ikicheza ugenini, Arsenal ikapata bao la kwanza dakika ya 24 mfungaji akiwa Mesut Ozil, goli lililodumu hadi mapumziko.

Dakika ya 72 na 80 Alexis Sanches akaifungia Arsenal mara mbili kabla Andy Carroll hajaipatia West Ham bao la kufutia machozi dakika ya 83.

Alex Oxlade-Chamberlain akaifungia Arsenal goli la nne dakika ya 84 huku Sanchez akikamilisha hat-trick yake kwa kuifungia Arsenal bao la tano dakika ya 86.

No comments