ARSENAL YAMKOSA JULIA DRAXLER BAADA YA KUKUBALI KUJIUNGA NA PSG


MASHAMBULIAJI Julian Draxler aliyekuwa akiwaniwa na Arsenal yuko njiani kujiunga na mabingwa wa Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG).

Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani tayari amekubali mkataba wa miaka minne PSG ingawa klabu yake ya Wolfsburg imesema mchezaji wake hataondoka bila pauni milioni 34 kuwekwa mezani.

Julian Draxler  mwenye umri wa miaka 23 amekuwa akiwaniwa na Arsenal katika kila dirisha la usajili.
No comments