ARSENE WENGER AJIPA MATUMAINI KWA MANENO YA BIBLIA BAADA YA KUPANGIWA NA BAYERN MTOANO LIGI YA MABINGWA

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger ametumia msemo wa biblia ili kumpa matumaini baada ya timu yake kupangiwa Bayern Munich kwenye mtoano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Arsenal kwa misimu sita imeshindwa kufika robo fainali ya mashindano hayo baada ya kutolewa kwenye mtoano.

Na kibaya zaidi ina rekodi mbovu dhidi ya Bayern Munich linapokuja suala la mashindano hayo ambapo imetolewa mara mbili kwenye hatua ya 16.

Hata hivyo Wenger ametumia mfano wa kitabu kitakatifu cha dini ya Kikristo cha biblia kwa kudai kuwa hata Mwenyezi Mungu alifanya kazi kwa siku sita na kupumzika siku ya saba.


“Kwa misimu sita tumeshindwa kufika robo fainali baada ya kufuzu kwa mtoano wa 16 bora. Tunasoma kwenye biblia kuwa Mungu alitumia siku saba kuumba dunia na sisi nasi mechi yetu ya Bayern ndio siku yetu ya saba,” alisema Wenger.

No comments