ARSENE WENGER ASEMA ANA WASIWASI NA JERAHA LA MATHIEU DEBUCHY

KOCHA wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa ana wasiwasi kuhusu jeraha alilopata nyota wake Mathieu Debuchy wakati wa mechi ya Jumapili katika michuano ya Ligi Kuu England.

Mechi hiyo dhidi ya Bournemouth ambayo waliondoka na ushindi wa mabao 3-1 ilikuwa ni ya kwanza kwa Debuchy, 31, kuichezea Genners tangu Nevomba mwaka jana ambapo walishinda 3-1 lakini akaumia misuli ya paja na kulazimika kuondoka uwanjani baada ya dakika 16 za mchezo huo.

Arsenal walishinda kupitia mabao mawili ya Alexis Sanchez na moja la Theo Walcott.


“Itanibidi nizungumze na watabibu lakini inaweza tu kujua hali halisi baada ya saa 48,” alisema Wenger.

No comments