Habari

ASHA BARAKA ASEMA FERGUSON NA ROGART HEGGA WAMEJIFUKUZA KAZI TWANGA PEPETA …Chokoraa na Kalala Jr mmh!

on

MKURUGENZI wa The African Stars Band ‘Twanga Pepeta” Asha Baraka
amesema Rogart Hegga na Ferguson si wanamuziki tena wa bendi hiyo.
Hatua hiyo imekuja baada ya wanamuziki hao kutangaza kuanzisha bendi
yao mpya DSS (Dar es Salaam Super Sound).
Asha Baraka amesema kamwe hawezi kuwa na wanamuziki ambao
wanazitumikia bendi mbili kwa wakati mmoja.
“Tulishakataa jambo kama hili wakati wanamuziki wetu waliposhiriki
kuanzisha Mapacha Watatu, msimamo wetu bado ni ule ule, Rogart na Ferguson
waondoke Twanga Pepeta wakaitumie kwa kujinafasi bendi yao mpya,” alisema Asha
Baraka katika maongezi yake na Saluti5.
Jumamosi iliyopita Rogart na Ferguson walitambulisha bendi yao mpya
lakini wakasema wao bado ni wanamuziki wa Twanga Pepeta na kwamba bendi hiyo ni
mradi wao wa pembeni wa kujiongezea kipato.
Lakini hilo limepingwa vikali na Asha Baraka na akasema hawahitaji
tena wanamuziki hao na amewaruhusu waondoke na nyimbo zao mpya walizotunga
wakiwa Twanga Pepeta … “Twanga Kwanza” ya Ferguson na “Mtu Makini” ya Rogart
Hegga.
“Nyimbo hizi bado hazijaachiwa hewani, tunawaruhusu waondoke nazo,
hatuzihitaji,” anaeleza Asha Baraka.
Wengine wanaokumbwa na rungu la Asha Baraka ni madansa wa kiume
Mapande na Maga ambao nao walitangazwa kuwemo kwenye DSS Band.
Mkurugenzi huyo wa Twanga Pepeta akasema kilichofanywa na wanamuziki
hao ni kinyume na taratibu za kazi na kimeonyesha utovu mkubwa wa nidhamu.
“Waliomba ruhusa ya kutosafiri na bendi wengine wakidai ni wagonjwa
lakini kumbe walikuwa na mipango yao ya kuhujumu bendi,” anaeleza Asha Baraka.
Kuhusu Chokoraa na Kalala Jr ambao nao hawakusafiri na bendi na badala
yake wakaenda kuwa mashuhuda wa utambulisho wa DSS Band, Asha Baraka amesema
suala lao litajadiliwa na menejimenti.
“Bado kuna utata kuhusu Chokoraa, alikuja kuonana na mimi leo mchana
na kusisitiza kuwa aliomba ruhusa kwa mkurugenzi msaidizi (Omar Baraka),  tutakaa pamoja na viongozi wa bendi na
kujadili suala lake yeye pamoja na la Kalala Jr ambaye naye ana utata kuhusu
ruhusa yake ya kutosafiri na bendi,” anafafanua Asha Baraka.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *