AUDIO: ASHA BARAKA APINGA WASANII WA TWANGA KUTUMIKA SHINDANO LA MARAPA WA BENDI …ni Chokoraa na Ferguson


MKURUGENZI wa Aset inayomiliki Twanga Pepeta Mamaa Asha Baraka “Iron Lady” amepinga vikali wasanii wa bendi yake kutumika kwenye shindano la marapa wa bendi Jumapili hii.

Tamasha la marapa wa bendi za dansi linafanyika siku ya X-Mas ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam, siku ambayo Twanga itakuwa Mbinga mkoani Ruvuma.

Miongoni mwa marapa waliotajwa katika tamasha hilo ni pamoja na Khalid Chokoraa na Ferguson (pichani) kutoka Twanga Pepeta.

Akiongea katika ofisi za Saluti5 mchana huu, Asha Baraka amesema ni marufuku kwa wasanii wao kushiriki onyesho hilo na badala yake amesema ni lazima wasafiri na Twanga Pepeta kwenda Mbinga.

Asha Baraka amesema: “Hatuwezi kuendesha muziki kihuni, tuna safari ya mikoani ambayo imelipiwa na promota, hakuna hata msanii mmoja aliyekuja kutuomba ruhusa ya kutokwenda mkoani Ruvuma. 

“Hatukatai wasanii wetu kufanya kazi zao binafsi lakini ni lazima waombe ruhusa na kutupa muda wa kutosha na sio kuandaa mambo kihuni.

“Msanii atakayeshiriki onyesho la Dar Live na kutoroka safari ya Mbinga, atakuwa amejiondoa kazini, hatutamhuitaji tena na atalazimika kutulipa kile tulichomlipa wakati wa kusaini mkataba wa kurejea Twanga Pepeta.

“Mzee Mbizo na King Dodoo ambao ndiyo wanaratibu show ya marapa wa bendi walikuja kwangu kutaka ushauri baada ya kukwama kumleta Defao siku ya X-Mas lakini hawakuniambia juu ya mpango wa kuweka show mbadala ambayo itahusisha marapa wa bendi. Wakaamua kunizunguka na kunichukulia wasanii wangu kinyemala.

“Nataka niwaambie kuwa mimi si mwanamke legelege, wajiandae kulipa fidia kwa promota aliyekodi show za mkoani Ruvuma na pia wajiandae kuwapatia ajira ya kudumu hao wasanii maana hatutawahitaji tena.”


Sikiliza audio ya Asha Baraka hapo chini.

No comments