Habari

BABY TALL AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI

on

DANSA wa zamani wa Twanga Pepeta na FM Academia, Baby Tall amefiwa na
mama yake mzazi  siku ya Alhamisi usiku.
Baby Tall (pichani kulia) ameithibitishia Saluti5 juu ya kifo cha mama
yake Bi Veronica Mwangosi (pichani kushoto) na kusema msiba uko nyumbani kwao
Tandale kwa Tumbo jijini Dar es Salaam.

Dansa huyo ambaye yuko Mombasa, Kenya amesema taarifa zaidi juu ya
mazishi zitatolewa baadaye na kwamba yeye anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam
Ijumaa hii saa 11 jioni.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *