BAO LA AGUERO NI “DHAHABU” KWA ATLETICO MADRID

ATLETICO Madrid inakula “kiulaini” kila mara Sergio Aguero akitupia bao wakati akiwa amevalia jezi ya Manchester City.

Manchester City ilipomsajili Aguero, moja ya vipengele kwenye usajili vilielekeza kuwa kila mara atakapofungia timu hiyo mabao 15 bado Atletico Madrid inatakiwa kulipwa kiasi cha pauni 210,000 (sh. mil 570).


Aguero tangu ameiunga na Manchester City mwaka 2011 amezamisha mabao 152 maanake ni kuwa Atletico Madrid imevuna kiasi cha pauni mil 38 (sh. bil 103).

No comments