BARNABA AWATAKA WASANII WENZAKE WASIFANYE MUZIKI WA KUBABAISHA

STAA wa muziki wa Kizazi Kipya, Barnaba amesema dunia  imebadilika na kwamba hakuna kufanya muziki wa kubabaisha na kuwataka wasanii  wanaoshindwa kwenda na wakati wakae pembeni na kufanya shughuli nyingine.

“Mashabiki wetu wanajua ni msanii gani anafanya vizuri na nani anafanya vibaya na hawawezi kudanganyika, hivyo wale ambao wamezoea wajue kwamba dunia ya sasa hakuna longolongo, mashabiki  wanataka vitu vya kweli,” alisema.

Barnaba alisema kuwa wasanii wanatakiwa kujituma kwa kufanyakazi zenye ubora na sio ubabaishaji ambao mwishoe watastukiwa na mashabiki na kukimbiwa.

Aliwataka wasanii wanzake kutambua kuwa muziki sasa unaelekea mahali pagumu pasipohitaji udanganyifu bali kufanya vitu vya ukweli ambavyo mashabiki wanavikubali.

No comments