BAYERN MUNICH WASEMA “HATUTAFANYA USAJILI WA SIFA!”

KIGOGO wa Bundelsliga na mabingwa watetezi wa Ujerumani, Bayern Munich wamesema hawana haja ya kufanya usajili kwa kuwaita kundini wachezaji wenye majina maalum kwani huo ni usajili wa sifa.

Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo kongwe, Matthias Sammer alithibitishia taarifa za kumsajili wenye majina makubwa katika dirisha la mwezi Januari mwakani.


“Ingawa tunahitaji kuwa na kikosi imara lakini tutaangalia idara chache sana za kuziba lakini siyo usajili mkubwa na wa kutisha,” alisema mkulugenzi huyo.

No comments