CARLO ANCELOTTI AWANIA SAINI YA AUGUSTO FENARNDEZ WA ATLETICO MADRID

MABINGWA wa tetezi wa Bundersliga Bayern Munich wanaichokoza klabu ya Atletico Madrid kwa kuwania saini ya kiungo mchezeshaji wa timu hiyo, Augusto Fernandez.

Bosi wa Bayern Munich, Carlo Ancelotti amenukuliwa akisema anamwania kiungo huyo raia wa Argentina kwasababu anatambua mchango wa wachezaji wanaocheza katika La Liga kwasababu ni Ligi ya mchakamchaka inayofanana na ile ya Bundesliga.

Fernandez ni aina ya wachezaji ambao wanaweza kucheza Ligi yoyote kutokana na umri wake na hata aina ya kiwango alichonacho.

Kiungo huyo amekuwa ni chaguo langu la awali na kama mambo yataonyesha kwenda sawa nitaangalia namna ya kumsainisha kiungo huyo mapema iwezekanavyo,". alisema bosi huyo.


Mabingwa hao watetezi wa Ujerumani wameweka nia hiyo baada ya kuridhishwa na kiwango cha kiungo huyo.

No comments