CHAZ BABA NA TWANGA PEPETA SASA NI KAMA MATE NA ULIMI


MWIMBAJI Chaz Baba ambaye ana mgogoro wa kimkataba na bendi ya Mashujaa Band, ni kama vile tayari mguu wake mmoja uko ndani ya Twanga Pepeta.

Kwa upande mwingine Mashujaa Band nayo imeonyesha wazi kuwa inajipanga na maisha mapya bila Chaz Baba tangu aliposusa kuendelea na kazi zaidi ya miezi mitano iliyopita.

Mara kadhaa Chaz Baba amekuwa akikwea jukwaa la Twanga kusalimia kisanii, lakini Ijumaa na Jumamosi ya wiki iliyopita, alishiriki program kamili ya bendi hiyo katika maonyesho yake yaliyofanyika Toroka Uje Tabata na Dar  Live Mbagala.

Saluti5 ilipomuuliza Chaz Baba katika ukumbi wa Dar Live iwapo amerejea Twanga Pepeta, alikataa na kusema bado hajajua hatma yake.

Kihistoria Chaz Baba aling’ara zaidi na Twanga Pepeta kabla hajajiunga na Mashujaa Band kwa uhamisho wa bei mbaya mwaka 2012.
 Chaz Baba akiitumikia Twanga Pepeta Jumamosi usiku
Chaz Baba (kushoto) sambamba na Chocky kwenye jukwaa la Twanga Pepeta Jumamosi usiku ndani ya Dar Live Mbagala
Picha hii ni ya Januari 12, 2012 Chaz Baba akipokewa na viongozi wa Mashujaa Band kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akitokea mapumzikoni Dubai na kutangazwa moja kwa moja kuwa msanii mpya wa bendi hiyo


No comments