CHELSEA YAICHAPA MANCHESTER CITY 3-1 NYUMBANI KWAKO ...Aguero alambwa kadi nyekundu


LILE swali la nani ataisimamisha Chelsea kwenye Ligi Kuu ya England bado halijapata jibu baada ya klabu ya Manchester City iliyokuwa inapewa nafasi kubwa ya kuibuka mbabe kukubali kipigo cha bao 3-1.

Kwa matokeo hayo Chelsea inazidi kutakata kileleni mwa msimamo wa Ligi na Diego Costa ndiye aliyekuwa mwiba kwa Manchester City kwa soka la hali ya juu alilolionyesha.

City iliyokuwa nyumbani, ilikuwa ya kwanza kupata bao kunako dakika ya 45 baada ya beki Gary Cahill kujifunga.

Diego Costa akaisawazishia Chelsea dakika ya 60 kabla Willian   hajatupia la pili dakika ya 70 huku Eden Hazard akifunga la tatu dakika ya 90 sekunde chache baada ya nyota wawili wa City Sergio Aguero na Fernandinho kulambwa kadi nyekundu.

MANCHESTER CITY: Bravo; Stones (Iheanacho, 78), Otamendi, Kolarov, Fernandinho, Gundogan (Toure 76), Navas, Sane (Clichy 69), Silva, De Bruyne, Aguero.

CHELSEA: Courtois; Azpilicueta, David Luiz, Cahill; Moses, Kante, Fabregas, Alonso; Pedro (Willian 49), Diego Costa (Chalobah, 81), Hazard (Batshuayi, 90+4).
Diego Costa produced a remarkable performance to help Chelsea secure a 3-1 victory away at Manchester City on Saturday

Diego Costa alikuwa msumari kwa Manchester City
Costa wheels away in celebration after equalising for the visitors with a fine finish with half and hour remaining in the match

Costa akishangilia bao la kusawazisha
Sergio Aguero was sent off for the hosts for a knee high challenge on David Luiz in the closing stages of the matchSergio Aguero alilambwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu mbaya ya goti David Luiz ukingoni mwa mchezo
Manchester City midfielder Fernandinho also saw red late on following an altercation with Chelsea midfielder Cesc FabregasKiungo wa Manchester City  Fernandinho naye akapewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Cesc FabregasNo comments