CHELSEA YAONGEZA KASI KUMFUKUZIA JOAO MARIO

IMEBAINIKA kuwa klabu tajiri ya Chelsea inaongeza kasi ya kumfukuzia nyota Joao Mario.

Siyo kumfukuzia tu wameshatangaza dau la kumng'oa ambalo ni pauni 50 mil.

Taarifa kutoka ndani ya The Blue zinasema kuwa kocha Antonio Conte ameweka katika orodha yake jina la kiungo huyo.

Kwa mujibu wa The Metro Conte amekuwa akimfuatilia kwa muda mrefu Mario mwenye umri wa miaka 25 na sasa ameamua kuweka wazi azma yake hiyo.

Akizungumzia usajili huo, Conte amesema anahitaji huduma ya kiungo huyo kama sehemu ya kuimarisha kikosi chake cha msimu ujao.

Aliongeza kuwa Mario ni kijana ambaye anapambana na kujiamini katika kikosicha timu yeyote hivyo kutua Chelsea ni sahihi kwa sasa.


“Nipo katika kusuka kikosi kipya kitakacho kuwa na wachezaji wapya na wazamani alizungumza Conte.

No comments