CHICHARITO AIKANA TENA MANCHESTER UNITED

JAVIER Hernandez maarufu kama “Chicharito” amekanusha kwa mara nyingi tetei zinazosema yu njiani kurejea Old Trafford.

Kisha akaweka bayana anachokiamini kwamba maisha ya soka ndani ya klabu yake ya sasa ya Borussia Monchengladbach ni ya mafanikio zaidi kuliko alipokuwa United.

Kauli ya Chicharito inakuja siku chache baada ya kuibuka kwa hoja kwamba kocha mpya wa United amepanga kufanya kila liwezekanalo ili aweze kumrejesha kundini ifikapo usajili wa majira ya kiangazi.

Akinukuliwa, amesema: “Ninajipongeza kwa hatua niliyoichukua ya kuondoka United na kutua katika Ligi ya Bundesliga ambayo imerejesha kiwango changu.”

“Nina jina kubwa hapa. Na kiwango changu pia kimepanda maradufu. Nimerudi katika chati yangu na jina langu hapa ni tofauti na lile la United ndani ya Primier.”

Kufuatia kiwango chake na mchango wake, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba – Desemba.

Hernandez alijiunga na Bayern Leverkusen katika usajili wa majira ya kiangazi kwa dau la dola mil 12 huku akiwa nahitjika kurejeshwa ikosini na ocha huyo Mreno.


Raia huyo wa Mexico alisajiliwa na kocha Alex Ferguson mnamo mwaka 2010 ambapo mara baada ya kustaafu kwa kocha huyo mkongwe akajikuta akipelekwa kucheza kwa mkopo Real Madrid.

No comments