CHRISTIAN BELLA APONDA BIFU LA DIMPOZ NA DIAMOND

MWIMBAJI wa muziki wa dansi Christian Bella ametaja jukwaa la wasanii kushindana kuwa ni tungo zinazokubalika na sio malumbano na matusi ya kudhalilishana kwenye mitandao ya kijamii.

“Ushindani katika muziki ni muhimu lakini sio kama huo wa Dimpoz na Diamond ambao kwa kweli unatia aibu kwa kutukanana hali ambayo inaweza kusababisha wakajishushia hadhi,” alisema Bella.

Alisema kuwa anasikitishwa kuona wasanii badala ya kushirikiana wanaanzisha uadui ambao hauchangii chochote kwenye muziki wao zaidi ya kujianika mitandaoni.


“Kuna baadhi ya wasanii wanasita kuzungumzia ugomvi huu wakidhani kwamba wanaukuza lakini ukweli ni kwamba sifurahishwi na ugomvi huu wa mitandaoni ambao unawafanya wasanii kurushiana maneno mazito na yenye kashfa," alisema.

No comments