CHRISTIAN BELLA SASA HATAKI TENA "KOLABO"... asema anahisi mashabiki wakamchoka haraka

MWANAMUZIKI nyota Christian Bella ambaye sasa amefungua Studio ya kurekodi muziki amesema ameanza kushtukia kushirikishwa katika nyimbo kwa vile anahisi kwamba huenda mashabiki wakamchoka haraka.

Alisema kuwa kwanzia sasa hawezi tena kuwa kila muda anaimba na kwamba atakuwa anaangalia kwanza kama kuna maslahi ndipo atakuwa tayari kushirikishwa.

“Haiwezekani kuimba kira mara ama kushirikishwa na kila msanii, cha msingi sasa nitakuwa kama kuna umuhimu kwangu kufanya hivyo lakini vinginevyo sitakuwa tayari bali nataka kolabo zenye faida kwenye muziki wangu,” alisema.


Bella amesema ameshabaini kwamba kolabo zinamfanya azidi kuzoeleka kwa mashabiki wake na hivyo kuonekana kama mtu wa kawaida na mwishowe watamchoka. 

No comments