CHRISTIAN BENTEKE ATAJWA KUWA NA "GUNDU"... makocha anaosajiliwa nao hufukuzwa baada ya muda mfupi

STAA Christian Benteke ni mkali wa kufunga ingawa sasa kuna rekodi yake nyingine ambayo itaanza kuwatisha makocha.

Benteke amechezea timu tatu za Ligi Kuu England ambazo zote makocha wake walifukuzwa baada ya kusajiliwa nao.
Paul Lambert, Brendan Rodgers na sasa Alan Pardew wameonja gundu la kumsajili Benteke.

Baada ya kung’ara nchini Ubelgiji, Benteke alisajiliwa na aston Villa wakati ikinolewa na Lambert.

Benteke alichezea kwa miaka mitatu chini ya Lambert ambaye baadae alifukuzwa.

Alijiunga na Liverpool baadae ambayo ilimsajili kwa kitita cha pauni mil 32.5.

Rodgers ambaye alikuwa anainoa Liverpool hakujua kuwa ndio alikuwa anatengeneza mazingira ya kuondoka katika klabu hiyo.

Kocha huyo alifukuzwa miezi mitatu tu baada ya kumsajili Benteke.

Benteke alibaki Liverpool kabla ya kusajiliwa na Crystal Palace iliyokuwa inafundishwa na Pardew.

Msimu huu alijiunga na Liverpool ambako hadi sasa amepachika mabao manane ambayo hayakusaidia kumlinda Pardew.

Pardew alifukuzwa Alhamisi iliyopita na kuendeleza mkosi wa kumsajili Benteke.

Palace ipo kwenye nafasi ya 17 kwenye ligi Kuu England ikikabiliwa na kibarua cha kujiokoa kushuka daraja.


Kocha mpya ya Crystal Palace ana kibarua kigumu ingawa atakuwa na uhakika wa kibarua chake kwani hakumsajili Benteke, gundu la benteke ni kwa kocha Yule anayemsajili kwenye kikosi chake ndio anaonja joto ya jiwe.

No comments