CHUCHU HANS ASEMA USHINDI WA TUZO ZA EATV UMEMUONGEZEA KASI YA KUANDAA MUVI KALI ZAIDI

BAADA ya kuwa miongoni mwa washindi wa tuzo za EATV, mwigizaji Chuchu Hans amesema kuwa ushindi huo umemuongezea kasi ya kukamilisha maandalizi ya filamu yake mpya ya "Cheupe."

Alisema kuwa alisitisha utoaji wa filamu hiyo baada ya kuwa miongoni mwa wasanii wanaowania tuzo hizo na sasa ameibuka na ushindi ambao anaamini umemuongezea kasi.

“Mimi nimeibuka n ushindi wa mwigizaji bora wa kike, ushindi huo umeniongezea ksi ya kukamilisha maandalizi yangu ya filamu ya "Cheupe" ambayo nilisiitisha baada ya kuwa mmoja wa wanaowania tuzo,” alisema.


Alisema angenyong’onyea iwapo angekosa ushindi lakini sasa amepata nguvu kwa kutambua kwamba kazi zake zinakubalika na kufafanua kuwa anataka filamu ya Cheupe iwe kali zaidi.

No comments