CONTE AMWAGA BIA ZA FURAHA YA CHELSEA KWA WAANDISHI WA HABARI

KATIKA kuonyesha furaha yake kwa jinsi timu yake inavyonyanyasa kwenye Ligi Kuu England, kocha wa Chelsea Antonio Conte alimwaga ofa ya bia kwa waandishi wa habari.

Conte aliwaalika waandishi wa habari kwa ajili ya kinywaji siku ya mkesha wa Sikukuu ya Krismasi.

“Alitualika kundi la waandishi wa habari kwenda kupata nae kinywaji siku moja kabla ya Sikukuu ya Krismasi. Tulifurahi kuwa nae kwa kweli,” Shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) lilieleza.

Conte alifuatana na waandishi hao kwenye baa moja iliyopo kwenye eneo la Cobham Surrey, nje kidogo ya jiji la London ambapo ndipo ulipo uwanja wa mazoezi wa Chelsea.


Kocha huyo anafurahi timu yake kuongoza Ligi hiyo na juzi alijisafishia njia ya ubingwa baada ya kuilaza Bournemouth mabao 3-0.

No comments