CONTE ASEMA KIPIGO CHA BOURNEMOUTH NI ONYO KWA WENGINE

KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte anaamini kitendo cha timu yake kuicharaza Bournemouth mabao matatu imekuwa onyo kwa timu nyingine za Ligi Kuu England.

“Nadhani leo tumetoa ujumbe mzito kwa timu nyingine,” alisema Conte baada ya timu yake kupata ushindi wa 12 mfululizo.

Conte alisema anafahamu kuwa watu wengine walikuwa wanasubiri kwa hamu kuona timu yake ikiboronga kwa kuwakosa wachezaji wakle muhimu Diego Costa na N’Golo Kante.

“Ushindi huu umedhihirisha kuwa wachezaji wote kwenye kikosi change wana uwezo,” aliongeza Conte.

Pedro alizamisha mabao mawili na Hazard kufunga bao moja la penati wakati timu hiyo ilipoibuka na ushindi huo.

Chelsea inakaribia kuikaribia rekodi ya Arsenal ya kushinda mechi 14 mfululizo za Ligi Kuu England.

Timu hiyo inaongoza Ligi Kuu England ikiwa na pointi 46 ikifuatiwa na Manchester United yenye 36.


Conte aliahidi kuwa timu hiyo itaendeleza nguvu ya kuhakikisha inashinda kila mechi.

No comments