DANEELE DE ROSSI AIKANA AS ROMA... asema hakuna mazungumzo yaliyofanyika kuhusu kuongeza mkataba

STAA mkongwe wa timu ya AS Roma Daneele De Rossi ameikana timu hiyo kuwa hakuna mazungumzo yoyote yaliyo fanyika kuhusu kuongeza mkataba wake na klabu hiyo ya Ligi ya Serie A na akasema kwa kwa sasa anatafakari wasiwasi wowote kuhusu hatima yake.

Mkataba wa sasa wa Rossi unatajiwa kumalizika mwiashoni mwa msimu huu na kuna wasawasi kuwa kiungo huyo mzaliwa wa jiji hilo la Roma mwenye umri wa miaka 33 hataongeza mingine.

Akizungumza baada ya kuhojiwa kuhusu jinsi hali ilivyo mara baada ya mechi ya mwishoni mwa wiki ambayo waliondoka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya timu ya Pescara ambapo alifikisha mechi ya 400 katika muchuano ya Ligi ya serie A Rossi alisema kuwa hadi sasa hakuna kitu kilichobadilika na hawezi kulizungumzia hilo.

“Kitu Pekee kinachoniumiza kichwa ni kuhusu msimamo wa Ligi, sitaki kuliangalia hilo kwa sababu nafahamu jinsi ilivyo kwa sasa tupo imara kuliko siku za nyuma na hilo ndilo la msingi vitu vingine sio muhimu katika kipindi hiki,” aliongeza staa huyo.


Kwa upande wake mkugenzi wa michezo wa AS Roma Mauro Baldissoni alisema hawana haraka kuhusu suala hilo la kumuongezea mkataba Rossi ambaye alitokea katika timu ya vijana mwaka 2001.

No comments