DAR LIVE KUSAKA RAPA BORA WA BENDI SIKU YA X-MAS …yupo Chokoraa, Ferguson, Kitokololo, G Seven


UPO uwezekano mkubwa wa bendi nyingi kukosa huduma ya marapa wao tegemeo wakati wa sikukuu ya X-Mas.

Hii inatokana na uwepo wa tamasha kubwa litakalohusu marapa wa bendi litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam Jumapili hii ya tarehe 25.

Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo Juma Mbizo, karibu marapa wote wa bendi wameshathibitisha kushiriki onyesho hilo la kumsaka rapa bora wa muziki wa dansi.

“Ni Tamasha kubwa ambapo kutakuwa na bendi maalum itakayowapigia ‘live’ marapa wote,” alisema Juma Mbizo.

Mratibu huyo ameiambia Saluti5 kuwa miongoni mwa marapa watakaoshiriki mtanange huo ni pamoja na Khalid Chokoraa, Ferguson, Mirinda Nyeusi, Totoo Kalala, G Seven, Kitokololo, Kabatano, Sauti ya Radi, Papy Catalogue na Hitler.

No comments