DAVID MOYES KUREJEA OLD TRAFFORD JUMATATU ...asema hata Klop na Guardiola wangeshindwa kuziba pengo la Ferguson


KOCHA wa zamani wa Manchester United David Moyes, anarejea Old Trafford Jumatatu huku akisema si Jose Mourinho, Carlo Ancelotti, Jurgen Klopp wala Pep Guardiola ambaye angeweza kuziba pengo la Sir Alex Ferguson.

Moyes anarejea Old Trafford akiwa kama kocha wa Sunderland ambayo itakuwa mgeni wa Manchester United kwenye mchezo wa Premier League utakaochezwa Boxing Day.

Kocha huyo aliyetamba na Everton, alimrithi Ferguson kiangazi cha mwaka 2013 lakini akadumu Manchester United kwa miezi 10 tu katika mkataba wake wa miaka sita.

Moyes amesema: “Sikutendewa haki lakini sijutii kilichotokea United, nadhani hata kwa watu kama Jose Mourinho, Carlo Ancelotti, Jurgen Klopp au Pep Guardiola ingekuwa ngumu kwao kupata mafanikio  punde tu baada ya kurithi nafasi ya Ferguson.

“Mancheaster United walikuwa na kikosi kizuri, lakini kulikuwa na wachezaji ambao walikuwa wanafikia ukingoni mwa soka yao, ilikuwa ni vigumu kuisuka upya timu kwa muda mfupi.”


No comments