DEAL DONE: MANCHESTER UNITED YAFANIKIWA KUMNASA VICTOR LINDELOF ...atakuwa beki ghali zaidi Old Trafford


VICTOR Lindelof ni kama vile ameshatua Manchester United katika usajili wa mwezi Januari baada ya Jose Mourinho kufanikiwa kumnasa kwa ada ya pauni milioni 42, linaandika The Sun la Uingereza.
Sentahafu huyo mwenye umri wa miaka 22 sasa atakuwa beki ghali zaidi Old Trafford. 
Rais wa Benfica Luis Filipe Vieira alipaa kwenda England kukamilisha mazungumzo baina ya Manchester United na kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Sweden ni kwamba klabu hizo mbili zimefikia muafaka.
Hata hivyo bado kuna utata juu ya ada iliyofikiwa, hii ni kutokana na Lindelof kuwaambia rafiki zake kuwa usajili wake wa kwenda Manchester United kwa pauni milioni 38 umekamilika.No comments